Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Fountain Gate FC imethibitisha mshambuliaji wao Yusuph Shabani Athuman (22), amejiunga na klabu ya Yangon United ya Myanmar baada ya Fountain Gate kufungiwa usajili na FIFA pamoja na TFF na kushindwa kumuingiza kwenye mfumo wa usajili.
“Hatukuweza kumtumia (Yusuph Athuman), kwa sababu tulishindwa kumuingiza kwenye mifumo ya usajili baada ya kufungiwa kusajili na ndio maana tulimtoa kwa mkopo kwenda Tanzania Prisons, lakini kama bahati kapata hiyo timu hiyo (Yangon United, Myanmar) na kufikia makubaliano ya kumpeleka huko, “
Kidawawa Tabitha, mtendaji mkuu wa Fountain GateYusuph Athuman aliwahi kupita vilabu kadhaa vya ligi kuu kama Biashara United, Young Africans SC, Coastal Union, West Armenia na Fountain Gate FC.
#NTTupdates