Na Mwandishi wetu.
Ikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kuanzia kwa michuano ya kombe la Dunia la vilabu la FIFA nchini Marekani, Mabingwa wa zamani wa ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Wydad Athletic club, imetangaza kuachana na Kocha mkuu wa kikosi hicho Rhulan Mlungis Mokwena (38) raia wa Afrika Kusini na nafasi yake ikichukuliwa na Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Amine Benhachem.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya klabu hiyo kushindwa kumaliza kwenye nafasi 2 za juu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Morocco (Botola Pro 1 league) na hawataweza kushiriki ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao na kuwafanya mabosi wa klabu hiyo kutoridhishwa licha ya kusalia kwa Michezo 3.
Mokwena alijiunga na Wydad Athletic club mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuachana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na amefanikiwa kuipandisha Wydad kutoka nafasi ya 7 ambayo walimaliza nayo kwenye ligi msimu uliopita hadi nafasi ya tatu msimu huu.
#NTTupdates