Na Mwandishi wetu.
Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaotarajia kumaliza elimu ya msingi wametakiwa kuwajengea mazingira rafiki yatakayowasaidia kutuliza akili zao na kuwawezesha kufanya vizuri pamoja na muwakumbushe kuwahi ratiba ya mtihani kwenye vituo vyao vya mitihani.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimu Msingi na Awali Wilaya ya Ukerewe Mwl. Bahati Dickson Mwaipasi wakati akitoa taarifa ya hali ya maandalizi ya mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi amewasihi wazazi na walezi wote wa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi unaotarajiwa kufanyika septemba 10 na 11 mwaka 2025 nchini Tanzania.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bukongo Mwl. Zengo Elikana Saguda amethibitisha kukamilika kwa maandalizi ya mtihani huo shuleni hapo huku akiwatia moyo watahiniwa wote kuwa wanaweza kufanya vizuri.”..
Maandalizi yamekamilika watoto wameandaliwa vizuri ndani ya miaka yote saba na wapo tayari kuukabili mtihani huo, tumewaambia wasiwe na hofu na wazingatie maelekezo ya mtihani ikiwa ni pamoja na maelekezo ya wasimamizi .”
Mwl. Saguda. Asteria Ramadhan Wilbert ni miongoni mwa watahiniwa wa shule ya Msingi Bukongo yeye ameahidi kufanya vizuri kwani amejiandaa vyema kwa mtihani huo .
Jumla ya watahiniwa 11,475 wavulana 5675 na wasichana 5800, miongoni mwao watahiniwa 35 ni wanafunzi wenye mahitaji maalum wanatarajiwa kufanya mtihani kwa masomo ya Kiswahili, Hisabati, Maarifa ya jamii na stadi za kazi, Kiingereza, Sayansi na teknolojia pamoja na somo la Uraia na Maadili.
Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya shule za msingi 140, shule 134 ni za serikali na shule sita ni za binafsi. Shule 133 ndizo zitakazofanya mtihani ambapo 130 ni za serikali shule tatu ni za binafsi.
#NTTupdates.