×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUWEKEZA NDANI YA NCHI.

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan, amewatakata wafanyabiashra na Watanzania wenye uwezo kuwekeza ndani ya nchi ili kutengeneza ajira na kukuza uchumi wa nchi kwa lengo la kuepuka utegemezi kutoka mataifa ya nje.

Rais Samia ametoa wito huo wakati akizungumza na Wananchi Mkoani Simiyu, mara baada ya kuzindua kiwanda cha mabomba na kuchakata pamba amesema malengo ya Serikali ni kuwafan ya wakulima wa zao la Pamba wanufaike ili waweze kujikwamua kiuchumi kwani sekta ya viwanda ina mchango mkubwa hapa nchini.

Amesema kwa kufanya hivyo, itasaidia watanzania wengi kujiepusha na kusubiri mikopo na misaada kutoka mataifa ya njee kwani jambo hilo linapelekea taifa kuwa tegemezi na kwa kufanya hivyo itaondoa utegemzi kwa wakulima.

Ziara ya Rais Samia Mkoani Simiyu inahusisha uzinduzi wa miradi sita ya kimkakati ambayo inalenga kuimarisha uchumi wa wananchi na kuleta maendeleo ya katika Mkoa huo.

#NTTUpdates