×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI WAOMBA KUONGEZWA SIKU ZA UTOAJI HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA WA SAMIA

Na Mwandishi wetu.

Wananchi mkoani Shinyanga wameiomba serikali Kuongeza siku za utoaji msaada wa Kambi ya Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia Kutokana na kile walichodai kuwa siku sita zilizowekwa hazitoshi kuwahudumia wananchi wote mkoani humo.

Wamesema tangu utoaji huduma uanze hadi kufikia siku ya leo June 25 ni siku ya tatu lakini wanamashaka kuwa Kutokana na umati mkubwa wa watu wanaohitaji huduma ni wengi hawatao hudumiwa wote.

Katika Kambi hiyo wapo Madaktari Bingwa wa watoto, wanawake, pua, koo na sikio, Madaktari Bingwa wa meno, Madaktari Bingwa wa magonjwa ya ndani ambapo wote hao wanalengo lakuhakikisha wanahudumiwa Wananchi hao wanapata huduma stahiki.

Kwa upande wake Daktari Moshi Ryoba amesema kwa siku wanapokea wananchi 167 ambapo kwa idadi ya kawaida upokea watu kati ya 50 adi 70 kwa siku hivyo jambo hilo si la kawaida kwani idadi ya watu wanaohitaji huduma ni wengi kulinganisha na hapo awali.

Naye Daktari Bingwa wa upasuaji kutoka hospital ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Daktari Boazi Mwasambili amesema kuwa pamoja na kuwa wakifanya kazi kwa ushirikiabo naadaktari Bingwa wengine waliopo katika Kambi hiyo lakini wakati mwingine wamekuwa wakimaliza kuwahudumia watu majira ya saa mbili usiku.

#NTTUpdates