×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI WANALITAKA KOMBE LAO

Na Mwandishi wetu.

Dakika 90 zimemalizika kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara na kushuhudia Wananchi Young Africans SC wakipata ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC na kuvuna alama 3 muhimu kwenye mchezo huo.

Magoli ya Young Africans SC yamefungwa na Clement Mzize aliyefunga magoli mawili dakika ya 39′ na 70′, kiungo mshambuliaji Aziz Ki dakika ya 43′ na mwamba wa Lusaka Cletus Chota Chama dakika ya 89′.

Ushindi huo umewafanya Young Africans kufikisha alama 70 baada ya kucheza michezo 26 huku mshambuliaji Clement Mzize akiwa kinara wa kupachika mabao akifunga magoli 13.

#NTTupdates