Na Mwandishi wetu.
Shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA – Taifa Tundu Lissu limeahirishwa na kusogezwa hadi Julai 15, Mwaka huu.
Hatua ya kuahirisha shauri hilo imefuata baada ya Mahakama ya Hakimu Moazi Kisutu, Jijini Dar es salaam kuafikiana na maombi ya upande wa Jamhuri ulioeleza kuwa Kwa Sasa bado hawajafanya uamuzi Wa kumshitaki rasmi Lissu Kwa makosa ya uhaini, shauri litakalofunguliwa Mahakama kuu.
wakati huo huo Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, Tundu Lissu ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iutake upande wa Jamhuri kulipeleka shauti lake Mahakama Kuu au Mkurugenzi wa Mashtaka atangaze nia ya kutoendelea na mashtaka yanayomkabili na kusisitiza kuwa hakuna haja ya suala hilo kuendelea kucheleweshwa huku akiendelea kusota magereza.
#NTTUpdates