×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TRY AGAIN AMWAGA MANYANGA SIMBA SC

Na Mwandishi wetu.

Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba SC Salim Abdallah maarufu kama Try again ametangaza rasmi kuachia ngazi kwenye klabu hiyo kama mwenyekiti wa bodi upande wa mdhamini wa klabu hiyo.

Tyr again alinukuliwa akisema “Kwa maslahi mapana ya Simba kwa kutambua mpira ni mchezo wa hisia, Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi nimemwomba Mwekezaji wetu Mohamed Dewji (MO) arejee kama Mwenyekiti wa Bodi nami nitasalia kama Mwanachama na Kiongozi ambaye nipo tayari wakati wowote kuitumikia Simba, kwa maana hiyo natangaza kuondoka kwenye kiti”

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa shinikizo kwa viongozi hao kuachia ngazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu ya Simba SC kwenye michuano ya Kitaifa na kimataifa.

Pia mwenyekiti huyo alishauri mwekezaji mwenye hisa nyingi kwenye klabu hiyo Mohamed Dewji (mo) kurejea kwenye nafasi yake ya kuwa mwenyekiti badala ya Rais wa heshima.

#NTTupdates