×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

THEO HERNANDEZ ATIMKIA AL HILAL SC YA SAUDI ARABIA

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Al Hilal SC ya Saudi Arabia imemtambulisha Theo Bernard Francois, Hernandez mlinzi wa kushoto wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Ufaransa kuwa mchezaji wao mpya akitokea AC Milan ya Italia.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, anaugana na nyota wengine wengi ambao awali waliwahi kutamba na vilabu vikubwa kwenye ligi na mashindano makubwa barani Ulaya na Sasa wanakipiga kwenye ligi kuu ya Saudi Arabia.

Theo Hernandez aliweka wazi kuwa alifanya mazungumzo na Joao Cancelo ambaye anakipiga Al Hilal SC, kabla ya kukubali ofa ya klabu hiyo na Cancelo alimwelezea sifa za klabu hiyo na mikakati mikubwa ambayo klabu hiyo imeiweka kwenye mashindano makubwa barani Asia.

Theo Hernandez amecheza jumla ya michezo 262, akifunga magoli 34 na kutoa assist 45 miaka yote wakati akiwatumikia klabu ya AC Milan.

#NTTupdates.