Na Mwandishi wetu.
Rais wa heshima na Mwekezaji wa klabu ya Simba SC Mohamed Dewji “MO” amemtetea Kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo, Jean Charles Ahoua (23), baada ya kukosa nafasi ya wazi dakika za Jioni kwenye mchezo wa Mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC), dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini na kuwafanya Simba SC wapate ushindi mwembamba wa 1-0.
Tajiri huyo amelifananisha tukio la Ahoua na matukio ya nyota wa zamani wa Liverpool, Fernando Torres ambaye alikuwa mchezaji hatari kwa wakati huo barani Ulaya.
“Jean-Charles Ahoua ni mmoja wa wachezaji waliotupa sababu nyingi za kushangilia msimu huu, licha ya vyote amekuwa sehemu ya mafanikio yetu”.
“Kwa kosa moja lilitokea tunaweza kumsema vibaya leo, ila tukumbuke: hata mastaa wa dunia kama Fernando Torres aliwahi kukosa magoli ya wazi kwenye mechi kubwa kama Chelsea dhidi ya Manchester United, Hii ni soka, Haya ni mambo ya kawaida kwenye mchezo huu.
Lakini jambo kubwa zaidi ni namna tunavyochagua kusimama baada ya kila tukio. Tunajifunza, tunaimarika, na tunaendelea kupambana.
“Mchezo wetu dhidi ya Stellenbosch bado uko mbele. Safari haijaisha. Na huu si wakati wa kulaumiana ni wakati wa kuungana na kuwa kitu kimoja”.
“Simba inajengwa juu ya mshikamano. Tunasimama na Jean-Charles. Tunasimama na kila mchezaji anayejitoa kwa jezi hii. Na tunaendelea na vita iliyokua mbele yetu”.
Ameyasema hayo baada ya mashabiki wa Simba SC kukerwa na namna kiungo mshambuliaji huyo alivyokosa nafasi ya wazi hapo jana, akiwataka waendelee kuwa na mshikamano.
#NTTupdates