Na Mwandishi wetu.
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeeleza kuwa tangu Mwezi Februari hadi Aprili Mwaka huu Kuna ongezeko la visa vya maambukizi ya ugonjwa Wa Uviko -19 nchini.
Amesema Takwimu zinaonyesha Katika kipindi hicho Kuna ongezeko la asimilia 1.4 ( wagonjwa 2 kati ya watu 139 waliopimwa), mwezi Februari hadi asilimia 16.3 (Wagonjwa 31 kati ya watu 190 waliopimwa) Mwezi Machi, na Kisha asilimia 16.8 ( Wagonjwa 31 kati ya Watu 185 waliopimwa) mwezi Aprili 2025.
Hayo yamewekwa wazi Katika taarifa yake Mganga Mkuu Wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema kuongezeka na kupungua Kwa Uviko-19 kumekuwepo Kila Mwaka tangu kutangazwa Kwa ugonjwa huo nchini Mwaka 2020.
#NTTUpdates