×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI YAONGEZA VYANZO VYA MAPATO KUPITIA MUSWADA MPYA WA FEDHA

Na Mwandishi wetu.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2025, ambao unafanya marekebisho katika sheria 33 mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuboresha mfumo wa ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya umma, kupunguza upotevu wa mapato na kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma.

Akiwasilisha muswada huo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa mabadiliko hayo yanagusa sheria mbalimbali zikiwemo Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147 na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha Sura ya 41.

Ameeleza kuwa mabadiliko hayo yamelenga pia kuimarisha Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote kupitia nyongeza ya tozo.

#NTTupdates