Na Mwandishi wetu.
Serikali imesema imebaini kuwepo Kwa wahalifu ambao wamefungua akaunti za Mitandao ya kijamii yenye majina yanayofanana na Taasisi zinazoaminika na kuchapisha maudhui ya upotoshaji na zenye kuzua taharuki.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Masigwa, kupitia ukurasa wake Wa Instagram, Amewataka Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wahalifu hao.
#NTTUpdates