×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RIBEIRO AAGA SUNDOWNS, AENDA HISPANIA

Na Mwandishi wetu.

Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) msimu uliopita Lucas William Ribeiro Costa (26), raia wa Brazil amewaaga rasmi mashabiki wa klabu ya Mamelodi Sundowns “The Brazilians” ambapo anatarajiwa kujiunga na CYD Leonesa inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania.

Ribeiro ambaye alijiunga na Mamelodi Sundowns mwaka 2023 akitokea klabu ya S.K Beveren ya Ubelgiji aliiteka mioyo ya mashabiki wa klabu hiyo kutokana na uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi kwa wenzake.

Msimu uliopita ulikuwa msimu bora kwa Ribeiro ambapo ndani ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) alibeba tuzo ya Kiatu cha Dhahabu baada ya kuwa mfungaji bora akiwa na magoli 16, MVP wa PSL, na goli bora la msimu huku nyota huyo ametwaa tuzo ya goli bora la Mashindano mapya ya Kombe la Dunia ngazi ya vilabu la FIFA 2025 nchini Marekani.

NTTupdates