×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC MTANDA AWAALIKA WANANCHI MAPOKEZI YA RAIS SAMIA MWANZA JUNE 19

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ametoa wito kwa wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaetarajiwa kuwasili Mkoani Mwanza kwa ziara ya siku tatu.

Kupitia taarifa aliyoitoa katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo juni 14, 2025 Mkuu wa Mkoa amesema Mhe. Rais Samia atawasili Mkoani Mwanza kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza siku ya jumapili, Juni 15, 2025 majira ya saa nane mchana ambapo atapokelewa na kisha kuelekea Mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi.

Aidha, Mhe. Mtanda amesema tarehe 19 Juni 2025 majira ya saa tano asubuhi, Mhe. Rais atawasili Mwanza akitokea Mkoa wa Simiyu na kisha kuanza rasmi ziara yake kwa kufungua Daraja la JPM lililopo eneo la Kigongo – Busisi, (Wilaya za Sengerema na Misungwi).

“Katika ufunguzi huo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapata fursa ya kuhutubia wananchi upande wa Kigongo (Wilaya ya Misungwi), katika Chuo cha Ufundi cha Kalwande”.

Mhe. Mtanda.“Tarehe 20 Juni, Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan atashiriki kwenye uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa chanzo kipya cha Maji na kituo cha kusafisha na kutibu Maji na kisha kushiriki kwenye Siku ya walinzi wa jadi (Sungusungu) katika Viwanja vya CCM Kirumba, ambapo pia tunawakaribisha wananchi kushiriki Mkutano huo.”

Amefafanua Mkuu wa Mkoa.“Katika siku hiyo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapata fursa ya kuhutubia wananchi kwenye viwanja hivyo vya CCM Kirumba”.

Ameendea kubainisha.Vilevile, Mkuu wa Mkoa ameendelea kwa kusema ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia itendelea tarehe 21, Juni ambapo atashiriki kama mgeni rasmi katika Tamasha la Utamaduni (Bulabo) litakalofanyika katika Viwanja vya Red Cross (Ngomeni) Kata ya Bujora Wilayani Magu.

Sambamba na utoaji wa ratiba hizo, Mkuu wa Mkoa amewataka wakazi wa Mkoa huo kushiriki katika matukio hayo lakini pia ametoa tahadhari ya kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika ziara hiyo na badala yake kuwa watiifu na wazalendo kwa kipindi chote ambacho Mhe. Rais atakuwepo Mkoani Mwanza.

#NTTUpdates