×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC MTANDA AKAGUA MAENDELEO YA UANDIKISHAJI WILAYA ZA KWIMBA NA MISUNGWI

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametembelea vituo vya uboreshaji wa daftari la Wapiga kura awamu ya pili katika Wilaya za Kwimba na Misungwi na kutoa wito kwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza kuendelea kutoa hamasa kwa Wananchi ili waweze kujitokeza.

Mhe. Mtanda amesema zoezi hilo ni muhimu kwa kuwa ndio hatua na kigezo cha awali kukidhi haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

“zoezi hili ni muhimu sana na linatoa nafasi kwa mwananchi kuhamisha taarifa, kurekebisha endapo watabaini dosari na kuwaandika upya wananchi waliokosa fursa wakati wa uandikishaji wa awali”.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kupitia vituo hivyo pia kuna ubandikaji wa orodha ya wananchi waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura, Hivyo amewataka wananchi kutembelea vituoni ili kufanya uhakiki wa taarifa zao.

“uwepo wa orodha hii pia ni kutoa nafasi kwa mwananchi kuomba kuingiza jina au kufuta jina la mpiga kura na kuweka pingamizi kwa mpiga kura alitepoteza sifa”. Ameongeza Mkuu wa Mkoa.

Uboreshaji wa daftari la wapiga kura awamu ya pili kwa Mkoa wa Mwanza umeanza leo Mei Mosi 2025 na utahitimishwa Mei 07, 2025 Zoezi hili la uboreshaji wa taarifa zimeenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la wapiga kura ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

#NTTUpdates