×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAIS MWINYI:SMZ KUENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za Kuimarisha Maslahi ya Watumishi ikiwemo Nyongeza ya Mishahara kuwepo kwa huduma ya Afya Ili kuchochea Utekelezaji Bora wa Majukumu Yao kwa dhamira ya kutoa huduma Bora kwa Wananchi.

Ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani 2025 yaliofanyika Viwanja vya Kizimkazi , Wilaya ya Kusini ,Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha Rais Dkt,Mwinyi amesema Serikali inatambua na kuthamini Kazi kubwa inayofanywa na Wafanyakazi Kuleta Maendeleo , Kukuza Uchumi na Ustawi wa jamii katika Sekta mbalimbali.

Akizungumzia Nyongeza ya Mshahara amewaahidi Wafanyakazi kuwa Serikali inaendelea na Mchakato wa kuangalia Uwezekano wa kuongeza Mshahara baada ya bajeti ya Serikali ya 2025-2026.

Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa Ushirikiano Uliopo Baina ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi umekuwa nyenzo Muhimu ya Utatuzi wa Changamoto zinazojitokeza katika Maeneo ya Kazi,Jambo alilolisisitiza kuendelezwa kwani linachangia Kuongeza Ufanisi.

Halikadhalika Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kufarijika na Mchango Mkubwa Unaotolewa na Wafanyakazi walioajiriwa katika Sekta rasmi na wale walio katika Sekta isio rasmi kwani Umefanikisha Utekelezaji wa Mipango mbalimbali ya Serikali na Maendeleo ya Nchi.Rais Dkt, Mwinyi ametoa Wito kwa Wafanyakazi Kuendelea kufanya Kazi kwa Uadilifu, Nidhamu na Uzalendo pamoja na kuwa Walinzi wa Amani iliopo hususani Mwaka Huu wa Uchaguzi Mkuu na kuwasisitiza kushiriki Uchaguzi kwa Amani kwa Maslahi ya Tàifa.

Awali Rais Dkt, Mwinyi aliyafunga Maonesho ya Wafanyakazi na Kuyapokea Maandamano ya Wafanyakazi waliobeba mabango yenye Ujumbe mbalimbali yenye mnasaba na Siku Hiyo ya Wafanyakazi Duniani iliobeba Kaulimbiu inayosema “Wafanyakazi Tufanye Kazi kwa biidii, Tudai haki kwa mujbu wa Sheria na tushiriki Uchaguzi kwa Amani.”

#NTTUpdates