
Na Mwandishi wetu.
MKUU wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga mapema Leo Agosti 14, 2024, amefanya ziara katika Shule mpya ya wasichana ya Manyara Girls, na kuongea na wanafunzi pamoja na kuwakaribisha rasmi Mkoa wa Manyara wanafunzi 110 waliokwisha wasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano (5) kwa mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB).
Pamoja ba hayo pia amewashukuru na kuwapongeza wazazi waliopeleka watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia watoto wao watapata elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwepo shuleni hapo.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa wa Manyara ameagiza umaliziaji wa miundombinu yote ambayo bado haijakamilika, ikamilike mapema ili wanafunzi waweze kupata huduma bora hasa umalizaji wa bwalo lililopo shuleni hapo.




#NTTupdates