Na Mwandishi wetu.
Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kushinda michezo yote mitatu ya hatua ya makundi Copa America 2024 baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Peru kwa jumla ya magoli 2-0.
Licha ya nyota wa Argentina Lionel Messi kutokuwepo kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Peru, lakini Argentina walicheza soka safi na kuendeleza makali yao.
Argentina imeingia tena kwenye rekodi ya kumaliza Kundi bila kupoteza mchezo wowote Copa America kama walivyofanya hivyo mwaka 1921.
Lautaro Martinez aliendeleza furaha na ushindi kwa Argentina baada ya kuingia kambani mara mbili akifunga magoli yote ya mchezo huo dakika ya 47 na 86 na kuwa kinara wa magoli Copa America akicheza michezo 3 na kufunga magoli 4.
Argentina pia wamemaliza hatua ya makundi bila kuruhusu goli lolote chinj ya kipa Bora wa michuano ya kombe la Dunia Emiliano Martinez.
Pia winga anayekipiga Man United Alejandro Garnacho alipata nafasi ya kuanza kwenye mchezo huo wa Copa America.
#NTTupdates