Na Mwandishi wetu.
Moto usiojulikana chanzo chake umeteketeza mbao za wafanyabishara katika soko la mbao eneo la sabasaba Mkoa wa Mwanza usiku wa kuamkia leo huku wafanyabishara thelathini wa soko hilo wakiathiriwa na amoto huo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo la mbao Idd Issa ambae mbao zake pia zimeteketea na moto huo anaeleza.
Mrakibu mwandimizi wa jeshi la zima moto na uokoaji Kaim kamanda wa jeshi hilo Mkoa wa Mwanza Elisha Kamugisha amesema kama zima moto wamefika eneo hilo kwa wakati ili kushibiti moto huo usilete madhara makubwa Zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda amefika eneo hilo na kutoa pole kwa waathirika wote na kuwataka kuwa na bima zitakazowasaidia wapatapo majanga ikiwemo majanga ya moto.
#NTTUpdates