Na Mwandishi wetu.
Dakika 90 zimemalizika kwenye uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar na kushuhudia Mnyama Simba SC akipata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) na kuifanya Simba SC kutanguliza mguu mmoja kwenye hatua ya Fainali ya kombe hilo msimu huu.
Goli pekee la Simba SC limefungwa na kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua na kupeleka furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo.
#NTTupdates