×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MNYAMA AMNYATIA DIARRASOUBA

Na Mwandishi wetu.

Taarifa zinaeleza kuwa Uongozi wa klabu ya Simba SC umeanza kufanyia kazi mapendekezo ya Kocha Fadlu Davis juu ya maboresho ya kikosi chao kuelekea msimu mpya kwa ajili ya mashindano ya ligi kuu ya NBC na ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Simba SC imefanya mazungumzo na kukubaliana na winga wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Asec Memosa, Salifou Diarrasouba ili ajiunge na miamba hiyo kwa msimu ujao.

Dili hilo likienda vizuri na kukamilika basi nyota huyo atatangazwa rasmi kuwa ni Mali ya Manyama Simba SC.

#NTTupdates