Na Mwandishi wetu.
Dakika 90 zimemalizika kwenye uwanja wa Berkane Municipal nchini Morocco na kushuhudia wenyeji RS Berkane wakifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mnyama Simba SC kwenye mchezo wa Mkondo wa kwanza fainali wa kombe la shirikisho Afrika (CAFCC).
Mnyama Simba SC anarejea nyumbani Tanzania kujiandaa na mchezo wa Mkondo wa pili ambao utapigwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar ambapo Mnyama atalazimika kushinda magoli zaidi ya matatu na kuizuia RS Berkane isipate goli ili waweze kubeba taji hilo.
#NTTupdates