×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MECHI YA HESHIMA NA UBINGWA

Na Mwandishi wetu.

Saa chache zimesalia kushuhudia mechi ya kibabe ya watani wa jadi kati ya Young Africans SC dhidi ya Simba SC katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam majira ya saa 11:00 Jioni.

Wananchi Young Africans SC ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo wametamba kubeba ubingwa wao wa 31 wa ligi kuu Tanzania bara na kuendelea kuweka historia na heshima ya kuwa mabingwa wa muda wote wa kombe hiloKwa upande wa Mnyama Simba SC, licha ya kuonekana wapo kimnya lakini wamejipanga kuwashangaza wapinzani wao kwa kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuweka historia ya kubeba taji mbele ya mahasimu wao.

Kariakoo Dabi ni miongoni mwa dabi mkubwa barani Afrika ambayo mara zote imekuwa ikiwavutia mashabiki na wadau wa soka wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

#NTTupdates.