Na Mwandishi wetu.
Washika mitutu wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) Arsenal FC, imemalizana na kumtambulisha mshambuliaji wao mpya Chukwunonso Azuka Tristan “Noni Madueke” mwenye umri wa miaka 23 raia wa Uingereza akitokea klabu ya Chelsea kwa dau la paundi milion 52.
Arsenal FC imempatia nyota huyo mkataba wa miaka 5 kuitumikia klabu hiyo ambapo ametia Saini na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mashindano mapya ya Fainali ya kombe la Dunia ngazi ya vilabu la FIFA ambapo Chelsea walifanikiwa kutwaa taji hilo.
Madueke ambaye msimu uliopita akiwa na Chelsea amecheza jumla ya Michezo 46, akifunga magoli 11 na kutoa assist 5 kwenye mashindano yote ambayo klabu hiyo ilishiriki, anaungana na kiungo mkabaji Zubimendi na goli kipa Kepa na wachezaji wengine kuipambania Arsenal ili iweze kuondoa uteja wao wa kushindwa kubeba mataji na kufanya vizuri zaidi msimu ujao.
#NTTupdates