×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MAANDAMANO YA KUMPINGA TRUMP YAPAMBA MOTO KATIKA MIJI YOTE MAREKANI

Na Mwandishi wetu.

Maelfu ya watu wamejitokeza katika miji mbalimbali kufanya maandamano kwenye miji mikubwa nchini Marekani, kupinga baadhi ya sera za Rais Donald Trump aliyeingia madarakani mwezi Januari mwaka 2025.

Miongoni mwa sera zake zinazopingwa na waandamanaji hao ni pamoja na za uchumi, kupunguzwa kwa wafanyakazi wa serikali, ushuru, uhamiaji na haki za binadamu.

Maandamano hayo ya Jumamosi yamefanyika katika maeneo 1,200 ya majimbo yote ya Marekani.

#NTTupdates