×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KILIMANJARO YAADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO KWA UPANDAJI WA MITI

Na Mwandishi wetu.

Mkoa wa Kilimanjaro umeadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa upandaji wa miti 15,000 katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro ( KIA) ikiwa ni hatua ya kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumzia zoezi hilo, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nudrin Babu amesema lengo kuu la kupanda miti hiyo ni kutunza mazingira ya kiwanja hicho pamoja na kukabiliana na mabadiliko yote ya tabianchi yanayoweza kujitokeza.

Babu amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro na nchi kwa ujumla umejikita katika kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabianchi na kuwataka wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanatumia mvua za masika kupanda miti.

Aidha, ametoa wito kwa wenyeviti wa vitongoji, vijiji na viongozi wa kata kuhakikisha wanaweka sheria ndogo ndogo za kuzuia mifungo kuingia katika maeneo yaliyopandwa miti hiyo ili lengo kuu liweze kutimia huku akiahidi kuwa mkali kwa yeyote atakayesababisha miti hiyo kuliwa na mifungo.

#NTTupdates.