×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KESI YA UHAINI YA LISSU NI HADI JULAI MOSI MWAKA HUU

Na Mwandishi wetu.

Shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema – Taifa, TUNDU LISSU limeahirishwa hadi siku ya Julai 1, Mwaka huu, ili kutoa nafasi Kwa mwendesha mashtaka Mkuu ( DPP), kuweza kupitia faili lake baada ya upelelezi kukamilika.

Hii Leo Mwenyekiti huyo wa CHADEMA – Taifa Aliomba Mahakama ajitetee mwenyewe huku akitaja sababu ni kuwa Mawakili wake kutopewa nafasi ya faragha kuzungumza naye gerezani.

LISSU anakabiliwa na kesi ya uhaini pamoja na ile ya kuchapisha taarifa za uongo Mtandaoni.Akiwa nje ya Mahakama hiyo Wakili Jebra Kambole ameeleza kuwa julai Mosi itajulikana kama shauri hilo litapelekwa Mahakama Kuu au lah.

Wakili Kambole amesema kuwa endapo DPP atakua amemaliza kulipitia faili la LISSU basi shauri litaenda mahakama Kuu na ikiwa bado itaelezwa Mahakamani hapo.

#NTTUpdates