×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KALI ONGALA ATUA KMC FC

Na Mwandishi wetu.

Watoza ushuru wa Manispaa ya Kinondoni KMC FC imemtambulisha Kalimangonga Sam Daniel Ongala Ramping (45) raia wa Uingereza kuwa Kocha wa kikosi hicho akichukua nafasi ya Abd Hamid Moallin aliyeondoka klabuni hapo hivi karibuni.

KMC FC imefikia makubaliano na Kocha Kali Ongala baada ya sintofahamu iliyojitokeza na Kocha wao Moallin ambaye anatajwa kujiunga na Wananchi Kali Ongala aliwahi kuiongoza Azam FC kama Kocha msaidizi pia alikuwa Kocha msaidizi wa Ngorongoro Heroes ambao walifanikiwa kubeba kombe la CECAFA U-20 na kufuzu michuano ya AFCON.

#NTTupdates