×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

JKT TANZANIA WAPATA AJALI YA GARI

Na Mwandishi wetu.

Timu ya JKT Tanzania inayoshiriki ligi kuu NBC imepata ajali ya gari leo na kupelekea majeraha kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi eneo la Mbweni baada ya basi la klabu hiyo kuacha njia na kuangukia Kwenye Mtaro.

Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Jemedari Said Kazumari kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo inaelezwa baadhi ya wachezaji wao ambao ni John Bocco, Dany Lyanga, Gamba Matiko, Said Ndemla, Mohamed Bakari, Hassan Kapalata, Yakouba Seleman na Salumu Gado wamepata majeraha na wapo hospitali kwa matibabu zaidi.

#NTTupdates