×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DKT.BITEKO AWASILISHA BUNGENI BAJETI WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2025/2026

Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ya kiasi cha shilingi Trilioni 2.2 ambapo asilimia 96.5 ya Bajeti yote ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na asilimia 3.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Akiwasilisha Bajeti hiyo leo tarehe 28 Aprili, 2025 bungeni jijini Dodoma, Dkt. Biteko ametaja vipaumbele mbalimbali vya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ikiwemo kuendelea kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, pamoja na kufikisha Gridi ya Taifa katika mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara.

“Mhe. Spika, kipaumbele kingine ni kuendelea na usambazaji wa nishati katika vitongoji, maeneo ya migodi, kilimo, viwanda na pampu za maji pamoja na vituo vya afya ili kuwezesha shughuli za uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.” Ameeleza

Dkt. BitekoAmetaja kipaumbele kingine kuwa ni upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kutekeleza Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa na kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Pia, kuhamasisha na kuwezesha watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) na Mpango wa Taifa wa Nishati wa Mwaka 2025 – 2030.

Dkt. Biteko ametaja kipaumbele kingine kuwa ni kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kutekeleza Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa na kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme.

#NTTupdates