×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC MKALIPA AKUTANA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MERU

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Wilaya ya Arumeru Amri Mohamed Mkalipa Septemba 11, 2024 amefanya kikao kazi na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Mkalipa, amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja ili kufanikisha malengo ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.

Pia amesisitiza kila idara ihakikishe inafikia lengo la ukusanyaji wa mapato na kuingiza taarifa ya asimilia kwenye mfumo kila mwisho wa mwezi wa ukusanyaji wa mapato ili kujua ni changamoto gani zinazowakwamisha kutimiza malengo.

Katika hatua nyingine, Mkalipa amezitaka Taasisi zilizoshiriki kwenye kikao hicho ikiwa ni pamoja na TARURA, TANESCO na AUWSA ambazo zinatoa huduma katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kutoa huduma inayostahili ikiwa ni pamoja na kutoka taarifa kwa wananchi pindi changamoto inapotokea ili kuepuka malalamiko.

#NTTupdates