×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

CHADEMA YATANGAZA MAANDAMANO ARUSHA

CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kimetangaza maandamano Mkoani Arusha yatakayofanyika Februari 27,2024 ikiwa ni muendelezo wa maandamano yaliyofanyika Dar es Salaam na Mwanza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya soko kuu lilipo jijini Arusha ,mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya kaskazini Godbless Lema amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kudai haki zao kupitia maandamano hayo.

Lema ameongeza kuwa wananchi wasiwe na hofu ili waweze kupigania katiba mpya na kukataa miswada ya sheria kandamizi iliyopelekwa bungeni kusainiwa kwa lengo la kuminya uhuru wa chaguzi mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu amesema maandamano hayo hayafungamani na dini,itikadi za vyama wala ukabila bali ni ya kudai unafuu wa maisha kwa kila mtanzania .