×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BARCELONA YAENDELEA KUMLIZA DON CARLO

Na Mwandishi wetu.

Kocha Mkuu wa kikosi cha Real Madrid Carlo Ancelott (65), raia wa Itali ameendelea kuwa na wakati mgumu kwenye michezo ya El classico baada ya kupoteza michezo 3 mfululizo dhidi ya FC Barcelona ambayo wamekutana msimu huu.

Real Madrid ilipoteza mchezo wa Fainali ya kombe la Mfalme (Copa del Rey) hapo jana kwa kipigo cha magoli 3 -2 na kuwafanya kusalia na kombe moja pekee la ligi kuu huku Kocha wa kikosi hicho Ancelott akiweka wazi kuwa matokeo ya mechi hiyo yamemuumiza na hawezi kuwalaumu wachezaji wake.

“Tulitawala kipindi cha pili na tulifanya kila tuliloweza. Siwezi kuikosoa timu yangu tulifanya bora, Nimeumia, tulikuwa karibu sana kushinda sasa tutazingatia kushinda La Liga”

Real Madrid iliondolewa kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA na Arsenal kwa kipigo cha jumla ya magoli 5-1, walipoteza mchezo wa fainali ya Supercopa dhidi ya FC Barcelona kwa magoli 5-2 na mchezo wa ligi kuu Hispania (La Liga) kwa magoli 4-0 msimu huu.

#NTTupdates