Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Barcelona imefanikiwa kutwaa taji la ubingwa wa kombe la Mfalme (Copa del Rey) baada ya kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid na kuweka rekodi ya kuwafunga mfululizo kwenye michezo 3 kwa vipigo vizito ndani ya msimu mmoja.
Magoli kwa upande wa Barcelona yalifungwa na Pedri dakika ya 28′, Ferran Torres dakika ya 84′ na J. kounde aliyefunga goli la ushindi dakika ya 116′ huku magoli ya Real Madrid yakifungwa na K. Mbappe dakika ya 70′ na A.
Tchouaman dakika ya 77′.Pia mchezo huo ulishuhudia Kadi tatu nyekundu kwa nyota wa Real Madrid ambao ni Mlinzi wa kati Rudiger dakika ya 120+3, Mlinzi wa kulia L. Vazquez dakika 120+3 na kiungo mshambuliaji Jude Bellingham 120+4.
Barcelona inaendelea kuweka historia ya kubeba taji la Copa del Rey mara nyingi zaidi ikiwa na makombe 32 huku wapinzani wao Real Madrid wakichukua mara 20.
#NTTupdates