×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BAKWATA ARUSHA WAMUOMBEA MAKONDA KUELEKEA UZINDUZI WA KAMPENI ZAKE.

Na Mwandishi wetu.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametembelea ofisi za Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Ofisi ya Mkoa wa Arusha na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Baraza hilo.

Mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo za Bakwata, Makonda amepokelewa na Viongozi wa Baraza hilo Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa, Shaaban Abdallah.

Katika mazungumzo yao viongozi hao walimtakia kheri kuelekea kwenye uzinduzi wa kampeni zake za Ubunge zitakazofanyika siku Ijumaa Septemba 12, 2025 katika Viwanja vya Soweto Jijini humo.

NTTupdates.