×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

AHMED ALLY “TIKETI ZENU MTAZITUMIA TAMASHA LA SIMBA DAY”

Na Mwandishi wetu.

Uongozi wa klabu ya Simba SC kupitia kwa Afisa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ally, amewataka mashabiki wa klabu ya Simba SC, kuzitunza tiketi walizonunua kwa ajili ya Fainali ya mkondo wa pili wa kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya RS Berkane ili wazitumie siku ya tamasha la Simba day ambalo linatarajiwa kufanyika mwezi Agosti (mwezi wa 8).

Simba SC walianza kuuza tiketi kwa mashabiki wao wakiamini mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, lakini CAF wamewataarifu kuwa mchezo huo utapigwa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar.

“Watu ambao tayari wameshakata tiketi za mchezo wa Simba dhidi ya Berkane kabla ya mabadiliko ya Uwanja watunze tiketi zao watazitumia kuingilia kwenye tamasha la SIMBA DAY mwezi wa 8”.

Amesema Ahmed Ally, Afisa habari wa klabu ya Simba kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Mei 20, 2025.

Simba SC watacheza mchezo wao wa mwisho dhidi ya RS Berkane siku ya Jumapili Mei 25 ,2025, kwenye uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar ambapo Simba SC watalazimika kupata ushindi wa magoli 3-0 ili wabebe taji hilo.

#NTTupdates