Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Barcelona imemtambulisha rasmi winga Marcus Rashford (27) kuwa mchezaji wao mpya wakimsajili kwa mkopo wa muda mrefu Hadi 2030 kutoka Manchester United huku kukiwa na kipengele cha kumnunua Jumla kwenye mkataba wake.
Nyota huyo ambae alipoteza namba kwenye kikosi cha kwanza kwa Makocha wawili, Mholanzi Erik Ten Hag na Mreno Ruben Amorim na kupelekea kupelekwa kwa mkopo West Ham United ambapo huko alifanya vizuri.
FC Barcelona imeamua kumsajili winga huyo baada ya kushindwa kumsajili nyota Nico Williams ambaye alikataa ofa ya kujiunga na klabu hiyo na kuamua kuongeza mkataba wa miaka 10 na Atletic Bilbao.
Rashford amekabidhiwa jezi namba 14 ambayo iliwahi kuvaliwa na Muingereza mwenzie mshambuliaji Gray Lineker ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Barcelona miaka ya 1986-1989.
#NTTupdates