Na Mwandishi wetu.
Serikali imeahidi kufikisha umeme katika shule ya ya msingi ya Lucas Mhina ili kurahisisha usomaji kwa wanafunzi pamoja na upatikanaji wa umeme kwa wanakijiji kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Akibainisha hilo Disemba 03, 2024 Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Sekta ya Nishati ndani ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
Kapinga amelielekeza Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kuhakikisha inafikisha umeme katika shule hiyo na Kijiji chote kwa ujumla wake kwani Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha kiasi cha shillingi million 300 kwaajili ya kupeleka umeme eneo hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga amesema kuwa Wilaya ya Monduli ina jumla ya kata 20, vijiji 62 na vitongoji 236 ambapo vijiji vyote tayari vimefikiwa na huduma ya umeme isipokuwa kwenye shule hiyo na maeneo jirani karibu na shule ambayo tayari Naibu Waziri wa Nishati ameshaitolea maelekezo.
#NTTupdates.