×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

KENANI ATOA SIKU TATU MADEREVA BODABODA KUONDOA FATAKI KWENYE BODABODA ZAO

Na Mwandishi wetu.

Madereva wa vyombo vya usafiri maarufu kama bodaboda mkoani Arusha, wametakiwa kuondoa fataki walizozifunga kwenye pikipiki zao, ambazo zimekuwa ni chanzo cha kelele na kero kwa wananchi pamoja na watumiaji wa usafiri huo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi akitoa siku tatu kwa waendesha pikipiki hao mara baada ya kujadiliana na madereva hao, kuhusu kero hiyo inavyolalamikiwa na wakazi na watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kwenye maeneo yote ya Mkoa huo.

Kenani ametoa rai hiyo, wakati alipofanya mkutano na madereva wa bodaboda, bajaji na maguta wa mkoa huo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Julai 22, 2025.

“Nimeletwa kero hii na wazee na viongozi wetu wa dini namila, unapopiga fataki hiyo kumbuka kelele hizo zinaleta kero kubwa kwa watu wanaosikia, kuna wagonjwa, kuna wazee na wengine wenye shida nyingine, fanyeni utaratibu wa kuondoa kifaa hicho mlichofunga, natoa siku 3 kama kuviondoa kama tulivyokubaliana hapa”. Amesema Kenani.

Hata hivyo amewataka madereva hao, kuheshimu na kuithamini kazi hiyo, kwani kazi hiyo kama kazi nyingine inayowaingizia kipato na kuendesha maisha yao na familia zao, hivyo akiwasihi kuhakikisha wanaendesha vyombo hivyo vya moto kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo.

“Tumieni kazi yenu kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, tumieni fedha vizuri kwa kuwa na malengo ya kimaendeleo, nyinyi ni vijana twendeni, twendeni tukafanye maendeleo.

hakikisheni Aidha, amewataka kuwa chanzo cha usalama wa mkoa wa Arusha kwa kuwa wao wapakia watu wa aina tofauti, na kuwataka kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo husika, kwa kuweka uzalendo mbele badala ya kudanganywa na kujihusisha na uhalifu.

#NTTupdates.