×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

HULK HOGAN WA WWE AFARIKI DUNIA

Na Mwandishi wetu.

Mcheza Mieleka maarufu Duniani Terry Gene Bollea akijulikana kama Hulk Hogan wa WWE amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 71.

Chanzo cha kifo cha nguli huyo inaelezwa kuwa alipata matatizo ya moyo nyumbani kwake huko Clearwater Florida na baadae alipelekwa hospital ya Morton Plant ambapo watoa huduma wa hospital hiyo walithibitisha kifo chake.

Watu mashuhuri duniani akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump na makamu wake JD Vance wameonyesha kusikitishwa na kifo hicho pia wanamieleka wenzie ambao ni Undertaker, Triple H na Ric Flair.

#NTTupdates