×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

DC KAGANDA AKUTANA NA WAKULIMA WAKUBWA BABATI, ATOA MAELEKEZO KWA AFISA KILIMO

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, leo Julai 25, 2025, amekutana na kufanya kikao maalumu na wakulima wakubwa wa eneo la Kiru pamoja na kupokea maombi na mapendekezo ya kuboresha sekta ya kilimo na mazingira katika eneo hilo muhimu kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Katika kikao hicho, wakulima hao wameishukuru Serikali ya Tanzania kwa hatua mbalimbali za kurejesha amani na kutatua migogoro iliyodumu kwa muda mrefu katika eneo hilo la Kiru, wakieleza kuwa, kwa sasa wanafanya shughuli zao kwa utulivu na amani pasipo shida yoyote huku wakiahidi kuendelea kuheshimu sheria za nchi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Kanganda amemuagiza Afisa Kilimo kuwasilisha taarifa ya kina kuhusu hali ya kilimo katika eneo hilo na mapendekezo ya hatua za kuendeleza sekta hiyo, ikiwemo miundombinu ya umwagiliaji, uhifadhi wa mazingira na ushirikiano na sekta binafsi.

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji hao katika kuhakikisha kilimo kinaendelea kuwa chanzo kikuu cha uchumi wa wananchi wa Babati.

#NTTupdates.