×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

BARCELONA YAMUENZI RONALDINHO

Na Mwandishi wetu.

Mabingwa wa ligi kuu ya Hispania (La Liga) msimu wa 2024/2025 klabu ya Barcelona kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, imemposti Aliyewahi kuwa Kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo, Ronaldo de Assis Moreira maarufu kama Ronaldinho Gaucho Raia wa Brazili, wakikumbuka siku waliyomtambulisha kwenye dimba la Camp Nou.

Siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, Ronaldinho Gaucho nguli wa soka alitambulishwa rasmi kama mchezaji wa Barcelona akitokea klabu ya PSG ya Ufaransa na tangu siku hiyo, tabasamu lake, uchawi wake uwanjani, na upendo wa mashabiki vilitengeneza enzi isiyosahaulika kwa mwamba huyo.

Ronaldinho aliitumikia FC Barcelona kuanzia mwaka 2003-2008 na alifanikiwa kutwaa tuzo kubwa Duniani upande wa soka kama Ballon D’or mwaka 2005, tuzo za FIFA na nyinginezo kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu na kuchezea mpira vile alivyokuwa anataka na kupeleka kubatizwa jina la “O Bruxo” likimaanisha Mchawi.

#NTTupdates